| Weka pombe sigara chini subiri tuongee |
| Zima kijiti marijuana za nini? Ngoja tuongee |
| Mbona ulisema mengi ukitaka nipotee |
| Sa umefanya nini? Na ulisema nini wala usijitetee |
| Macho hayana pazia |
| Nilimwona navutia |
| Naye kanikubalia |
| Kumbe moyoni unaumia |
| Dunia imejaa visanga |
| Ubinadamu umekuwa majanga |
| Tembo amefungwa kwa banda |
| Anataka kula kuku pia na vifaranga |
| Mungu tu akusamehe |
| Wewe ni kama ndugu yangu |
| Upunguze ma ugali |
| Uadui wa nini mwenzangu we |
|
| Ukitenda kosa na haujaomba radhi unakosea (Kosea) |
| Mama yake mzazi huruma ungemwonea (Mwonea) |
| Chunga kinywa kiwe na kituo |
| Hekima ndo iwe funguo |
| Maneno ya nini? Unajivua nguo |
| Kumbuka ulimwengu ni kama chuo |
|
| Ungenyamaza, bora ungenyamaza |
| Kaa kimya kama huna la maaana |
| Ungenyamaza, bora ungenyamaza |
| Ukikosa heshima bora kukaa kimya |
| Ungenyamaza, bora ungenyamaza |
| Bora ungenyamaza |
| Ungenyamaza tu, bora ungenyamaza |
| Kuwa muungwana |
|
| Mmmmh hasira hasara |
| Mimi ni ndugu yako kanitoa kafara |
| Ukakesha hukutaka kulala |
| Ukipambana niharibikiwe kaka wa Mtwara |
| Ukasahau mapenzi ni siri |
| Tena siri ya wawili |
| Kilichokuponza maadili |
| Tamaa ukashindwa isitiri |
| Tunza heshima yako |
| Na mashabiki wako hadi mbungeni |
| Na unapotongoza warembo |
| Boxer usiweke pembeni |
| Macho hayana pazia |
| Nilimwona navutia |
| Naye kanikubalia |
| Kumbe moyoni unaumia |
|
| Ukitenda kosa na haujaomba radhi unakosea (Kosea) |
| Mama yake mzazi huruma ungemwonea (Mwonea) |
| Chunga kinywa kiwe na kituo |
| Hekima ndo iwe funguo |
| Maneno ya nini? Unajivua nguo |
| Kumbuka ulimwengu ni kama chuo |
|
| Ungenyamaza, bora ungenyamaza |
| Kaa kimya kama huna la maaana |
| Ungenyamaza, bora ungenyamaza |
| Ukikosa heshima bora kukaa kimya |
| Ungenyamaza, bora ungenyamaza |
| Bora ungenyamaza |
| Ungenyamaza tu, bora ungenyamaza |
| Kuwa muungwana |
|